Idadi ya waliofariki kwa mvua Korea Kusini yafikia watu 40
17 Julai 2023Katika mji wa Kati wa Cheongju, mamia ya waokoaji wakiwemo wapiga mbizi, waliendelea kuwatafuta manusura kwenye handaki lenye matope ambapo takriban magari 15, likiwemo basi, yalikwama kwenye mafuriko ambayo huenda yalijaza njia ya handaki hilo kwa muda wa dakika Jumamosi jioni.
Kufikia sasa miili 13 imeopolewa na majeruhi tisa kupata matibabu.
Haikubainika mara moja idadi ya watu waliokuwemo katika magari yaliyozama.
Soma pia:Zaidi ya watu 30 wamefariki katika mafuriko Korea Kusini
Katika ripoti yake, wizara ya mambo ya ndani na usalama imesema takriban nyumba 200 na barabara 150ziliharibiwa kote nchini humo huku watu 28,607 wakikosa umeme kwa siku kadhaa zilizopita.
Takriban watu 40 wamekufa, wengine 34 kujeruhiwa na zaidi ya 10,000 kulazimika kuhama kutoka makazi yao tangu Julai 9, mvua kubwa ilipoanza kunyesha nchini humo.