1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waliouawa Sudan wafikia 400, majeruhi wapindukia 3,500

21 Aprili 2023

Shirika la Afya Duniani (WHO) linasema zaidi ya watu 400 wameuawa na wengine zaidi ya 3,500 kujeruhiwa katika mapigano yanayoendelea nchini Sudan baina ya vikosi vya jeshi rasmi na jeshi la dharura.

https://p.dw.com/p/4QPhr
Sudan Khartum | Kämpfe | Fliehende Menschen
Picha: Ebrahim Hamid/AFP/Getty Images

Msemaji wa shirika hilo, Margaret Harris, aliwaeleza waandishi wa habari mjini Geneva kwamba vituo 20 vya afya vimesimama kufanya kazi na vingine 12 viko katika hatari ya kuacha kutoa huduma.

Harris aliongeza kuwa hali hiyo sio tu inaathiri watu waliojeruhiwa wakati wa mapigano, bali pia wale waliokuwa wakihitaji matibabu hapo kabla.

Soma zaidi:Wasudani waadhimisha Eid-ul-Fitr katikati ya mabomu 

Nalo Shirika la Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) limedokeza pia kwamba watoto tisa ni miongoni mwa waliouawa na 50 wamejeruhiwa.

Msemaji wa UNICEF, James Elder, amesema kwamba mapigano ya Sudan yamechangia familia nyingi kukwama majumbani zikiwa hazina umeme, chakula, maji na madawa.