Wanaharakati waandamana viwanja vya ndege Ujerumani
13 Julai 2023Maandamnao hayo yalitatiza usafiri wakati ambapo msimu wa likizo ndefu katika majira ya joto unaendelea.
Msemaji wa polisi amesema shughuli za ndege zilisimamishwa katika uwanja wa Hamburg tangu saa 12:00 asubuhi baada ya watu tisa kuingia katika eneo la uwanja wa ndege bila idhini na kujilaza kwenye barabara ya kurukia ndege.
Hivi sasa polisi wanajaribu kuwaondoa watu hao kutoka kwenye eneo hilo.
Safari za ndege kadhaa kwenye uwanja wa Hamburg zimefutwa.
Soma zaidi: Polisi Ujerumani wawahamisha wanaharakati kupisha mgodi wa makaa
Katika uwanja wa ndege wa Dusseldorf ulio magharibi mwa Ujerumani, safari zimeanza tena baada ya watu saba kuingia uwanjani bila idhini na kujilaza kwenye barabara ya kurukia ndege.
Waandamanji wa kundi la Letzte Generation mara kwa mara huzuia magari barabarani na kutatiza shughuli kwenye viwanja vya ndege nchini Ujerumani.