Wanajeshi 4 wa Israel wafariki nchini Lebanon
9 Desemba 2024Jeshi la Israel limesema wanajeshi hao walikuwa askari wa akiba wenye umri kati ya miaka 25 na 43.
Vyombo vya habari vya Israel vimeripoti kwamba wanajeshi hao wa akiba walikuwa wakitekeleza majukumu yao kwenye eneo hilo.
Israel na wapiganaji wa kundi la Hezbollah la nchini Lebanon walisimamisha mapigano kuanzia mwishoni mwa Novemba, lakini mivutano mikubwa bado inaendelea na pande mbili hizo zinalaumiana juu ya kuyakiuka makubaliano yaliyofikiwa.
Israel inaendelea kushambulia upande wa kaskazini mwa Lebanon mara kwa mara.
Wakati huo huo, Israel imefanya mashambulio ya anga kwenye maeneo yanayotuhumiwa kuhifadhi silaha za kemikali na makombora ya masafa marefu ili kuzuia silaha hizo kuingia katika mikono ya watu wenye misimamo mikali.
Pia imeteka eneo ndani ya Syria ili kujihakikisha usalama ndani ya nchi hiyo baada ya wanajeshi wa Syria kuondoka.