WASHIGTON : FBI yakiri kukiuka sheria za faragha
10 Machi 2007Matangazo
Wabunge wa Marekani wanafikiria hatua ya kuchukua baada ya Shirika la Upelelezi la Marekani FBI kukiri kukiuka sheria za faragha nchini Marekani wakati wakifanya uchunguzi wa ugaidi.
Ukaguzi uliofanywa na Idara ya Sheria umeonyesha kwamba FBI ilikuwa na hatia ya kutumia vibaya sana madaraka yao kwa ajili ya kupata habari za binafsi kwa siri kama vile mawasiliano ya simu ya kibinafsi,baruwa pepe na rekodi za fedha.
Umoja wa Uhuru wa Kiraia wa Marekani unatowa wito wa kutenguliwa kwa madaraka yaliongezewa shirika hilo la FBI chini ya Sheria ya Patriot ambayo imepitishwa baada ya mashambulizi ya kigaidi ya Septemba 11 nchini Marekani.