WASHINGTON. Paul Wolfowitz ateuliwa rais mpya wa benki ya dunia.
1 Aprili 2005Matangazo
Benki ya dunia imemteua Paul Wolfowitz kuwa rais wake wa kumi, licha ya baadhi ya mataifa wanachama kuonyesha wasiwasi wao kuhusu jukumu lake katika vita vya Irak. Makamu huyo wa waziri wa ulinzi wa Marekani, anaichukua nafasi ya James Wolfensohn, ambaye anastaafu baada kuingoza benki hiyo kwa muongo mmoja. Wolfowitz ameahidi kulifuatilia lengo la benki hiyo la kupambana na umaskini duniani. Amelaumiwa kwa kukosa ujuzi wa maswala ya maendeleo na jukumu lake katika vita vya Irak. Wolfowitz ameyakaribisha maendeleo ya kiuchumi ya China na akasema ulimwengu unatakiwa kushirikiana na umma wa China licha ya kutokubaliana na siasa za taifa hilo.