WASHINGTON: Robert Zoellick aidhinishwa rais wa Benki ya Dunia
26 Juni 2007Matangazo
Bodi ya magavana wa Benki Kuu ya Dunia,kwa kauli moja imepiga kura kumuidhinisha Mmarekani,Robert Zoellick kama rais mpya wa wa benki hiyo.Paul Wolfowitz aliekuwa rais wa Benki Kuu ya Dunia, alikubali kuondoka madarakani mwezi uliopita,baada ya jopo maalum kuamua kuwa kiongozi huyo alikwenda kinyume na sheria za benki, alipompandisha cheo mpenzi wake na kumpatia nyongeza kubwa ya mshahara takriban miaka miwili iliyopita.