SiasaSyria
Watawala wapya wa Syria wateua waziri wa mambo ya kigeni
21 Desemba 2024Matangazo
Hayo yameripotiwa na shirika la habari la Syria (SANA) likinukuu taarifa iliyootolewa na kamandi tawala ya nchi hiyo inayoongozwa na mkuu wa kundi la waasi wa Hayat Tahrir al-Sham Ahmed al-Sharaa.
Shibani, mwenye umri wa miaka 37 na mhitimu wa chuo kikuu cha Damascus, aliwahi hapo kabla kuongoza idara ya siasa ya serikali ya waasi kwenye jimbo la kaskazini magharibi la Idlib.
Chanzo kimoja kilicho sehemu ya utawala mpya wa Syria kimeliambia shirika la habari la Reuters kuwa uteuzi wa Shibani umefanyika kama sehemu ya azma ya watu wa Syria kuanzisha mahusiano ya kimataifa ili kuleta amani na uthabiti.