Watu 11,000 wakimbia makaazi yao kusini magharibi mwa Niger
13 Julai 2023Matangazo
Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Uratibu wa Masuala ya Kiutu (OCHA) mjini Niamey imesema watu hao wanakimbia machafuko yanayofanywa na makundi ya watu wenye silaha.
Ghasia hizo zinatokea kwenye mkoa wa Tillaberi na eneo la mpaka unaozikutanisha nchi tatu za Niger, Burkina Faso na Mali.
Soma zaidi: Mamia ya watu waathirika na mafuriko na kipindupindu huko Cameroon na Chad
OCHA imesema watu waliyakimbia makaazi yao baada ya mauaji ya wanakijiji wawili usiku wa Julai 3.
Baadhi yao walilazimika kulala kwenye vyumba vya madarasa na wengine walihifadhiwa na familia zingine.
Niger imekumbwa na uasi wa wanamgambo wenye itikadi kali wanaofanya mauaji na kuwateka raia.