Idadi ya waliokufa kwa mripuko Lebanon yafikia 37
19 Septemba 2024Matangazo
Kwenye mkutano na waandishi wa habari katika mji mkuu Beirut, Waziri wa Afya Firas Abiad amesema takriban watu 3,000 wamejeruhiwa katika milipuko hiyo. Mamia ya vifaa vya kielektroniki vinavyotumiwa kwa ajili ya mawasiliano na wanamgambo wa Hezbollah viliripuka jana na leo. Ingawa Israel haitangaza wazi kuhusika, inalaumiwa na kundi hilo ambalo limeapa kulipiza kisasi.