Mafuriko yasababisha vifo, watu kukosa makazi Ulaya ya Kati
15 Septemba 2024Matangazo
Takriban watu 1,600 wamehamishwa kutoka eneo hilo na mamlaka za Poland zimeomba msaada wa jeshi kusaidia uokoaji.Mtu aliyekufa kutokana namvua hizo Kaskazini mashariki mwa Austria ni mwanamume aliyekuwa mfanyakazi wa idara ya zimamoto.
Soma zaidi: Ulaya ya Kati yakumbwa na mafuriko
Huko Jamhuri ya Czech, polisi wamesema, watu watatu waliokuwa kwenye gari lililozolewa na maji na kutumbukia kwenye mto katika mji wa Lipova Lazne hawajulikani walipo. Mwanamume mwingine ametoweka baada ya kusombwa na mafuriko eneo la kusini mashariki.
Nako Kusini mashariki mwa Romania, watu wanne wamekufa na miili yao imepatikana katika eneo lililoathiriwa vibaya zaidi na mafuriko la Galati. Takriban nyumba 5,000 zimeharibiwa kutokana na mvua hizo.