1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu kiasi 13 wafa kutokana na mafuriko Uhispania

Josephat Charo
30 Oktoba 2024

Watu wapatao 13 wamekufa kutokana na mafuriko yaliyotokea kusini mashariki mwa Uhispania. Taarifa hiyo imeripotiwa na shirika la utangazaji la kitaifa TVE hivi leo likiwanukuu polisi.

https://p.dw.com/p/4mOPR
Mafuriko ya Uhispania
Mafuriko ya Uhispania Picha: Alberto Saiz/AP Photo/picture alliance

Watu wapatao 13 wamekufa kutokana na mafuriko yaliyotokea kusini mashariki mwa Uhispania. Taarifa hiyo imeripotiwa na shirika la utangazaji la kitaifa TVE hivi leo likiwanukuu polisi.

Saa chache kabla, kiongozi mkuu wa eneo la Valencia aliwaambia waandishi habari kwamba idadi isiyofahamika ya maiti zilikuwa zimepatikana lakini hakutoa takwimu kwa kuziheshimu familia za wahanga.Watu kadhaa wamekufa kutokana na mafuriko Ulaya ya kati

Mvua kubwa katika eneo la kusini na mashariki mwa Uhispania zilimesababisha mafuriko barabarani na mijni jana Jumanne, na kuwalazimu maafisa wa eneo hilo kuwashauri raia wabaki majumbani na kuepuka safari zisizo za lazima.