1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiMarekani

Waziri wa Fedha wa Marekani asema uchumi hautadodora

8 Aprili 2023

Waziri wa fedha wa Marekani Janet Yellen amesema ana matumani kuwa uchumi wa taifa hilo utaendelea kukua licha ya wasiwasi wa kutokea mdodoro kufuatia msukosuko ulioikumba sekta ya benki hivi karibuni.

https://p.dw.com/p/4PptH
Waziri wa Fedha wa Marekani, Janet Yellen
Waziri wa Fedha wa Marekani, Janet Yellen Picha: Andrew Caballero-Reynolds/AFP/Getty Images

Kwenye mahojiano na shirika la habari la AFP, Yellen amesema uchumi wa Marekani ambao ndiyo mkubwa duniani utaendelea kushamiri ikiwa ni pamoja na kukua kwa soko la ajira na kupungua kwa mfumuko wa bei.

Matamshi yake yanafuatia wiki kadhaa za mtikisiko nchini Marekani baada ya kufilisika kwa benki kubwa mbili hali iliyoibua mashaka ya kutokea mzozo wa kifedha kama ulioikumba dunia mnamo mwaka 2008.

Ingawa serikali ya Marekani iliingilia kati kutuliza wasiwasi uliotokea, wakuu kadhaa wa taasisi za kifedha nchini humo wamesema taathira za kuanguka kwa benki hizo zitaendelea kuonekana kwenye uchumi kwa miaka kadhaa inayokuja.