Waziri Svenja Schulze, kukutana na viongozi wa ECOWAS
4 Februari 2024Matangazo
Ziara ya Schulze inafanyika juma moja baada ya mataifa ya Burkina Faso, Mali na Niger ambayo yanatawaliwa kijeshi kuziondoa nchi zao katika jumuiya hiyo kwa kile walichodai jumuia hiyo ipo chini ya ushawishi wa mataifa ya kigeni ambayo yanatishia uhuru wao.
Watawala hao wa kijeshi walisema katika tamko lao la pamoja kwamba Jumuiya ya ECOWAS pia iliweka vikwazo "visivyofaa" na "visivyo vya kiutu" kufuatia mapinduzi yaliofanywa dhidi ya serikali za kiraia.
ECOWAS ina nchi wanachama 15, na kuifanya kuwa moja ya jumuiya kubwa zaidi za kiuchumi za kikanda barani Afrika.