Waziri wa mambo ya ndani wa Uingereza ziarani nchini Rwanda
19 Machi 2023Matangazo
Braverman ametembelea eneo la Bwiza kunakojengwa kituo cha kuwapokea wahamiaji hao na kusema makubaliano kati ya Uingereza na Rwanda yatasaidia kutafutia suluhu ya haki na kibinaadamu katika suala la wahamiaji.
Kigali na London walifikia makubaliano ya dola milioni 146. Mwaka jana, zaidi ya wahamiaji 45,000 waliwasili kwenye pwani ya Kusini-Mashariki mwa Uingereza wakitumia mashua ndogo, ikiwa ni ongezeko la asilimia 60 kila mwaka tangu mwaka 2018.
Soma pia: Kagame na Sunak wazungumzia mkataba juu ya wahamiaji
Serikali na Upinzani nchini Uingereza wamekuwa wakitofautiana juu ya mpango huo ambao unaweza kuamuliwa kwenye Mahakama ya Juu ya Uingereza baadaye mwakani. Hadi sasa, mpango huo haujaanza kutekelezwa.