Haiti: Ghasia za magenge nchini ''ni sawa na eneo la vita''
26 Januari 2024Geneus ameliambia baraza hilo kwamba haijapita miaka miwili ambapo anakuja tena mbele ya baraza hilo kuchora picha ambayo ni ya kusikitisha zaidi na ambayo ni ya giza kila wakati ya hali ya usalama na kibinadamu nchini Haiti.
Watu wa Haiti wamechoka
Genus ameongeza kuwa watu wa nchi hiyo hawawezi kuvumilia zaidi na anatumaini kwamba hii ni mara ya mwisho atakayozungumza kabla ya kupelekwa kwa kikosi hicho cha kimataifa kuwasaidia maafisa wa usalama nchini humo.
Hakuna tofauti kati ya ukatili nchini Haiti na ukatili wa vita na mizozo ya silaha
Geneus amesema ikiwa Haiti itachapisha takwimu za kila siku kuhusu kile alichosema ni ukatili unaofanywa dhidi ya Wahaiti na magenge yenye silaha, watu wataelewa kwamba hakuna tofauti kati ya ukatili wanaovumilia na vitisho na ukatili wa vita na mizozo ya silaha mahali pengine, ambayo imevutia hisia za dunia.
Kenya yapiga hatua katika maandalizi ya kupeleka kikosi chake Haiti
Balozi wa Kenya katika Umoja wa Mataifa Martin Kimani, amesema serikali yake inapiga hatua muhimu katika maandalizi ya kupeleka maafisa wake katika misheni hiyo.
Soma pia:Viongozi wa makundi ya uhalifu Haiti wawekewa vikwazo
Haiti imeshuhudia ukosefu wa usalama kwa miaka mingi, uliochangiwa na mauaji ya rais Jovenel Moise mwaka wa 2021.
Soma pia:Haiti kujadili na Kenya juu ya kupelekwa askari
Ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa siku ya Jumanne, imesema kuwa magenge sasa yamekithiri katika maeneo mengi nchini humo na mauajiyameongezeka kwa zaidi ya mara mbili mwaka jana kufikia takriban 4,800.