1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Waziri wa mambo ya nje wa Italia azuru Beijing

Josephat Charo
5 Septemba 2023

Waziri wa mambo ya nje wa Italia Antonio Tajani anafanya ziara ya siku tatu Beijing ambako amekutana na maafisa wa Italia na kuandaa zira ya waziri mkuu wa Italia Georgia Meloni.

https://p.dw.com/p/4VxNt
Italien | Treffen Wang Yi mit Antonio Tajani
Picha: Angelo Carconi /ZUMAPRESS/picture alliance

Waziri wa mambo ya nje wa Italia Antonio Tajani amekutana na waziri wa mambo ya nje wa China Wangi Yi mjini Beijing. Waziri Wang amesema leo baada ya kukutana na Tajani hapo jana kwamba China na Italia zinatakiwa zizingaitie njia sahihi za kushirikiana na kufanya kazi pamoja kupitia kuheshimiana, uwazi na ushirikiano, huku mahusiano baina ya nchi hizo mbili yakiwa msitari wa mbele katika uhusiano kati ya China na Umoja wa Ulaya.

Waziri Wang amesema China na Italia zinatakiwa kwa pamoja zilinde mfumo huru na ulio wazi wa biashara, kudumisha mnyororo imara wa ugavi wa kimataifa, na kutoa mazingira ya haki ya biashara kwa kila mmoja. Waziri Tajani aliwasili Beijing siku ya Jumapili kwa ziara ya siku tatu inayokamilika leo, huku akikutana na maafisa wa Italia na kuandaa ziara ya waziri mkuu wa Italia Giorgia Meloni nchini China.