1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUrusi

Waziri wa Mambo ya Nje wa Korea Kaskazini aelekea Urusi

29 Oktoba 2024

Waziri wa Mambo ya Nje wa Korea Kaskazini, Choe Son Hui, ameelekea Moscow, ikiwa ni ziara yake ya pili nchini Urusi katika kipindi cha wiki sita.

https://p.dw.com/p/4mKXq
Sergei Lavrov na Choe Son Hui walipokutana Pyongyang 2023
Korea Kaskazini inatuhumiwa kwa kutaka kuingia katika vita vya Urusi na UkrainePicha: Russian Foreign Ministry/REUTERS

Shirika la habari la Korea Kaskazini limesema ujumbe ulioongozwa na Chie uliondoka jana kwa ziara rasmi nchini Urusi, bila kufafanua.

Choe ameelekea Moscow wakati Jumuiya ya Kujihami ya NATO ikiungana na Korea Kusini na Marekani katika kuthibitisha kuwa Korea Kaskazini imepeleka wanajeshi nchini Urusi.Inasema vikosi vya jeshi la Korea Kaskazini vilipelekwa katika eneo la Urusi la Kursk kwenye mpaka na Ukraine. Wizara ya Ulinzi ya Marekani imesema Washington haitaweka vizuizi vipya kwa Kyiv kutumia silaha za Kimarekani kama Korea Kaskazini itaingia katika vita vya Moscow dhidi ya Kyiv. Ilisema Korea Kaskazini imepeleka askari 10,000 mashariki mwa Urusi kwa ajili ya mafunzo.

Soma pia: Kansela Olaf Scholz wa ujerumani ahofia kutumwa wanajeshi wa Korea kaskazini nchini Ukraine

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO, Mark Rutte amesema kuongezeka kwa ushirikiano wa kijeshi kati ya Urusi na Korea Kaskazini ni kitisho kwa usalama wa eneo zima la Indo Pasifiki pamoja na kanda ya Ulaya, mataifa ya Caucasus na Asia ya Kati.