Waziri wa Nje wa Uingereza ziarani Marekani
6 Desemba 2023Ziara hiyo inayolenga kuthibitisha mahusiano imara kati ya mataifa hayo mawili lakini pia kusisitiza umuhimu wa msaada na ufadhili kwa Ukraine.
Waziri mkuu huyo wa zamani anatazamiwa pia kusisitiza umuhimu wa Uingereza na Marekani kuendelea kuiunga mkono Ukraine dhidi ya uvamizi wa Urusi.
Tangu kuanza kwa uvamizi huo Februari mwaka jana, Bunge la Marekani tayari limeshaidhinisha zaidi ya dola bilioni 110 kwa ajili ya Ukraine.
Soma zaidi: Umoja wa Ulaya kutayarisha vikwazo vipya dhidi ya Urusi
Lakini tangu Warepublican walipochukua udhibiti wa Baraza la Bunge mwezi Januari, wamekuwa wakizuia misaada zaidi ya kufadhili vita hivyo.
Uingereza imetangaza kifurushi kingine kwa Ukraine cha dola milioni 36.52 katika msimu huu wa baridi na itatoa pia dola milioni 9.76 kwa ajili ya misaada ya kibinaadamu.