Waziri wa zamani wa fedha wa Ujerumani afariki dunia
27 Desemba 2023Matangazo
Wolfgang Schaeublealitoa mchango mkubwa katika majadiliano ya kuungana upya Ujerumani mbili, ya Mashariki na Magharibi mwaka 1990, na kama waziri wa fedha wakati wa utawala wa Kansela Angela Merkel, alikuwa kiungo muhimu katika juhudi za kubana matumizi zilizosaidia kuiondoa Ulaya katika mgogoro wa madeni zaidi ya miongo miwili baadae.
Soma pia:Bunge la Ujerumani kufanya kikao chake cha kwanza
Baada ya miaka minane ya kushikilia washiwa wa waziri wa fedha chini ya serikali ya Kansela wa zamani Angela Merkel, Schaeuble alichukuwa mikoba ya kuwa spika wa bunge la Ujerumani hadi mwaka 2021, ambao ni wadhiwa wa mwisho alioushikilia katika safari yake ya kisiasa nchini Ujerumani.