Westerwelle ajiuzulu
4 Aprili 2011Kufuatia matokeo mabaya ya chama chake katika chaguzi za mikoa, Westerwelle amesema kuwa hatogombea tena wadhifa huo, ambao ameushikilia kwa miaka kumi mfululizo.
Kura za FDP zimeshuka hadi 5% tangu chama hicho kilipojiwekea rikodi ya kufikia 14% miaka miwili iliyopita.
Katika siku za karibuni, viongozi wa FDP wa mikoa wamekuwa wakimshutumu waziwazi Westerwelle.
Kamati Tendaji ya FDP inakutana leo, ingawa hadi sasa hakujatajwa mtu makshusi wa kushika nafasi ya uenyekiti.
Westerwelle amekumbana na upinzani mkali baada ya Ujerumani kujizuia kupiga kura kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa katika azimio la marufuku ya anga dhidi ya Libya. Hatua inaonekana kuitenga Ujerumani na washirika wake, ikiwemo Marekani.
Vile vile, FDP iliukana msimamo wake kuhusu nyuklia baada ya maafa ya Fukushima nchini Japan.