WFP yafikisha msaada wa chakula Darfur
6 Aprili 2024Matangazo
Kulingana na Umoja wa Mataifa takribani watu milioni 25, ambao ni zaidi ya nusu ya idadi ya watu wa Sudan, wanahitaji msaada wa haraka, ikiwa ni pamoja na karibu milioni 18 ambao wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula.
Soma zaidi: WFP: Machafuko ya Sudan yanaweza kusababisha mgogoro wa kikanda
Msemaji wa WFP nchini humo, Leni Kinzli, alisema misafara miwili ya misaada ilivuuka katika eneo la magharibi kutoka nchi jirani ya Chad ikiwa imebeba msaada wa chakula na lishe kwa watu wapatao 250,000 wanaokabiliwa na njaa kali.
Msemaji wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Margaret Harris, aliwaambia waandishi wa habari kuwa mahitaji ya kibinaadamu nchini Sudan ni makubwa sana.