Mkutano wa mwaka wa WHO waanza Geneva
27 Mei 2024Wanachama 194 wa WHO wanapanga kuanzisha miongozo ya vipaumbele vya miaka minne ijayo, ikiwa ni pamoja na mpango wa kuiondoa kabisa Malaria katika baadhi ya mataifa ifikapo 2030, lakini pia hatua ya kukabiliana na ongezeko linaloibua kitisho la usugu wa bakteria, fangasi, virusi, na vimelea.
Hafla ya kutiliana saini mkataba wa WHO kuhusu majanga, iliahirishwa baada ya miaka miwili ya kujadiliwa kwa miaka miwili na kuhitimishwa Ijumaa iliyopita bila ya makubaliano.
Wahusika kwenye majadiliano hayo walishindwa kuafikiana kuhusu masuala nyeti kama vile usambazaji wa dawa, vifaa vya kinga na chanjo wakati kunapotokea majanga huko siku za usoni.
Kusanyiko hili la sasa linatarajia kuamua juu ya hatua zinazofuata kuelekea kufikia mkataba wa kimataifa.
Soma pia: WHO: Mataifa yakamilishe mkataba wa kudhibiti majanga
MAfunzo yaliyopatikana kutokana na janga la UVIKO-19 yanatarajiwa kujadiliwa kwenye mkutano huo. Lakini pia kukiwa na matarajio ya kufanyika marekebisho kadhaa ya kimataifa ya WHO ikiwa ni pamoja na kupitishwa kwa kanuni na sheria mpya za kuzuia kuenea kwa magonjwa katika mipaka ya nchi pamoja na wajibu wa kutoa taarifa za milipuko kwa WHO mara moja.
Kaulimbiu ya mkutano wa mwaka huu wa WHO ni "Afya kwa Wote."
Soma pia:WHO yatahadharisha juu ya uhaba wa chanjo ya kipindupindu