WTO yatamatisha mkutano bila kufikia makubaliano muhimu
2 Machi 2024WTO ilichelewesha kilele cha mkutano huo mjini Abu Dhabi kwa zaidi ya siku moja wakati jumuiya hiyo ya kimataifa yenye wananchama 166, ikipambana kufikia muafaka juu ya sekta ya uvuvi, kilimo na masuala mengine muhimu. Makubaliano pekee yalioafikiwa ni ya kurefusha usitishaji wa kodi kwenye vyombo vya habari vya kidigitali.
Mkurugenzi wa Mkuu wa shirika hilo la Biashara Ngozi Okonjo-Iweala amesema mkutano huo umefanyika katika hali ambapo dunia imekumbwa na "mashaka makubwa" kuliko wakati wowote ule.
Soma pia:Mkutano wa WTO hauna dalili za makubaliano
Katika ufunguzi wa mkutano huo siku ya Jumatatu Ngozi hakugusia moja kwa moja mzozo wa Israel na Hamas, lakini alitaja usumbufu unaoendelea wa meli za kibiashara katika Bahari ya Shamu unaosababishwa na wapiganaji wa Kihouthi.