Zaidi ya watu milioni 7 kukabiliwa na njaa Sudan Kusini
1 Mei 2024Shirika la FAO limesema kiwango cha juu zaidi cha njaa cha asilimia 65 na 75 ya idadi jumla ya watu kinaripotiwa katika jimbo la kaskazini la Unity, Upper Nile, Jonglei na pia kwenye mkoa wa mashariki mwa Sudan Kusini wa Pibor karibu na mpaka na Ethiopia na miongoni pia mwa raia wa Sudan Kusini wanaorejea nyumbani kutoka nchi inayokabiliwa na vita ya Sudan.
Shirika hilo la chakula na kilimo limesema sababu zinazopelekea usalama mdogo wa chakula nchini humo ni changamoto za kiuchumi zilizosababisha viwango vya juu vya mfumuko wa bei, usambazaji mdogo wa chakula, mafuriko na migogoro
Sudan Kusini nchi changa kabisa duniani, iliyopata uhuru wake kutoka Sudan mwaka 2011, pia imekuwa ikipambana kuzijumuisha pamoja pande mbili hasimu za jeshi, kuandaa katiba mpya, na kutayarisha pia uchaguzi wake kwa nza mwezi Desemba mwaka huu.