1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zelensky ahimiza mpango wa F16 uharakishwe

26 Agosti 2023

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amewatolea wito washirika wake kuharakisha mpango wa kuipa Ukraine ndege za kisasa za kivita chapa F-16, ili kulisaidia jeshi la nchi hiyo kujilinda dhidi ya mashambulizi ya Urusi.

https://p.dw.com/p/4VbuZ
Ukraine | Unabhängigkeitstag in Kiew | Wolodymyr Selenskyj
Picha: kyodo/dpa/picture alliance

Katika vidio iliyotumwa kwenye mitandao ya kijamii, Zelensky alisema kundi lake la kimataifa linafanya kazi kutanua mafunzo ya utumiaji wa ndege hizo haraka iwezekavyo. 

Mapema wiki hii Denmark na Uholanzi ziliridhia kutoa ndege hizo kwa Ukraine baada ya Zelensky kufanya ziara fupi huko. 

Zelensky ayashukuru mataifa ya Ulaya kwa ahadi za misaada

Awali Waziri wa Ulinzi wa Ukraine Oleksiy Reznikov, alisema wanajeshi wa Ukraine wameanza kufunzwa namna ya kutumia ndege hizo, na mafunzo hayo huenda yakachukua miezi sita au zaidi kukamilika. Ndege aina ya F-16 zitaanza kusafirishwa baada ya mafunzo hayo kukamilika.