Zimbabwe yawalilia wafadhili na wakopeshaji wa kimataifa
4 Mei 2020Waziri huyo amesema katika barua iliyoandikwa Aprili pili iliyolifikia shirika la habari la Reuters leo Jumatatu kwamba Zimbabwe inahitaji kuanza mazungumzo na kurudisha uhusiano wa kawaida na wakopeshaji wakigeni ili kuyamaliza malimbikizo yake ya madeni ya miongo kadhaa na kufungua fursa ya kupata fedha za haraka zinazohitajika.
Ncube ameleeza kwenye barua yake kwamba maofisa nchini Zimbabwe wanapendekeza uwepo mdahalo wa ngazi ya juu kuhusu kuzuia hali mbaya zaidi ya kiuchumi na kijamii kutokea nchini humo kufuatia janga la ugonjwa wa Covid-19.
Barua hiyo imetumwa kwa shirika la fedha la kimataifa IMF na benki ya dunia pamoja na benki ya maendeleo ya Afrika,benki ya uwekezaji ya Ulaya miongoni mwa taasisi nyingine za fedha.Wakopeshaji kama IMF na benki ya dunia zilisita kuipa mkiopo Zimbabwe mwaka 1999 baada ya nchi hiyo kushindwa kurudisha mkopo huo.