SiasaAzerbaijan
Azerbaijan yafanya uchaguzi wa rais
7 Februari 2024Matangazo
Rais wa sasa na mwenye ushawishi mkubwa Ilham Aliyev anatazamiwa kwa kiasi kikubwa kujishindia muhula wa tano madarakani.
Ukandamizaji wa vyombo huru vya habari na kutokuwepo upinzani wowote wa kweli dhidi ya Aliyev, vinamuongezea uhakika wa kupata ushindi wa kishindo. Mwezi Septemba mwaka jana, Vikosi vya Baku vilichukua tena udhibiti wa eneo linalozozaniwa la Nagorno-Karabakh.
Vyama vikuu vya upinzani katika taifa hilo lenye utajiri mkubwa wa mafuta vimesusia uchaguzi huo. Kiongozi wa chama cha upinzani cha National Front, Ali Kerimli ameutaja uchaguzi huo kama "maigizo ya demokrasia" na kusisitiza kwamba hali ya sasa nchini Azerbaijan, hairuhusu kufanyika kwa uchaguzi huru na wa haki.