1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaNigeria

Boko Haram yaua watu 37 katika shambulio la kigaidi Nigeria

3 Novemba 2023

Kundi la kigaidi la Boko Haram limeshambulia mwanzoni mwa wiki hii na kuwaua wanakijiji 37 katika wilaya ya Geidam katika Jimbo la Yobe kaskazini mashariki mwa Nigeria.

https://p.dw.com/p/4YMms
Wanamgambo wa Boko Haram wamekuwa wakifanya mashambulizi yanayosababisha maafa ya raia nchini Nigeria na pia visa vya utekaji nyara wananchi.
Wanamgambo wa Boko Haram wamekuwa wakifanya mashambulizi yanayosababisha maafa ya raia nchini Nigeria na pia visa vya utekaji nyara wananchi.Picha: Issouf Sanogo/AFP/Getty Images

Waasi hao wa itikadi kali za kiislam waliwaua watu 17 kwa kuwapiga risasi huku wengine 20 wakifariki kwa bomu la kutegwa ardhini.

Uasi wa Boko Haram ulioanza mwaka 2009 nchini Nigeria na uliojikita katika jimbo la Borno lililo karibu na Yobe, tayari umesababisha vifo watu 35,000 huku wengine zaidi ya milioni 2 wakilazimika kuyahama makazi yao.

Rais wa Nigeria Bola Tinubu, ambaye aliingia madarakani mwezi Mei, hajafanikiwa kumaliza matatizo ya kiusalama katika taifa hilo lenye watu wengi zaidi barani Afrika.