1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chama cha mrengo wa kulia chashinda Austria

30 Septemba 2024

Chama cha mrengo mkali wa kulia nchini Austria kinachoongozwa na Herbert Kickl, Freedom Party, kimepata ushindi wa kwanza wa kihistoria katika uchaguzi wa bunge la kitaifa.

https://p.dw.com/p/4lETp
Herbert Kickl Austria
Kiongozi wa chama cha mrengo wa kulia cha Freedom Party nchini Austria, Herbert Kickl.Picha: Johann Groder/EXPA/picturede/picture alliance

Chama hicho kiliutumia wasiwasi uliokuwepo miongoni mwa wapiga kura kuhusu uhamiaji, mfumuko wa bei, vita vya Ukraine na masuala mengine muhimu katika kampeni zake.

Matokeo ya awali yanaonesha chama hicho kinashika nafasi ya kwanza kwa kupata asilimia 29.2 ya kura na chama cha kihafidhina cha Kansela Karl Nehammer cha Austrian People's Party kikiwa kwenye nafasi ya pili kwa kupata asimilia 26.5 ya kura.

Soma zaidi: Chama cha Freedom chashinda uchaguzi wa bunge Austria

Chama cha siasa za wastani za mrengo wa kushoto, Social Democratic, kimeshika nafasi ya tatu kikiwa na asilimia 21 ya kura.

Serikali ya mseto inayoondoka madarakani ya vyama vya Austrian People's Party na Cchama cha Kijani, imepoteza wingi wake katika bunge.

Chama cha Freedom Party kimesema kiko tayari kuzungumza na vyama vingine vya siasa ili kuunda serikali ya mseto.