1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Christian Lindner atoa wito kwa Wasiyria warudi kwao

25 Desemba 2024

Aliyekuwa waziri wa fedha wa Ujerumani Christian Lindner ametoa wito kwa wakimbizi wa Syria walioko Ujerumani kurejea nchini mwao baada ya kuanguka ghafla kwa uongozi wa muda mrefu wa Bashar al-Assad

https://p.dw.com/p/4oZZA
FDP stellt in Berlin ihr Programm für vorgezogene Neuwahlen vor
Picha: Nadja Wohlleben/REUTERS

Lindner amesema kwa wale waliokuja nchini Ujerumani kutoka Syria kwa sababu ya vita vya wenyewe kwa wenyewe, kurudi nyumbani inapasa iwe sheria. Hata hivyo waziri huyo wa zamani ameeleza kuwa wale wanaotaka kubakia wanaweza kuomba hifadhi ya kudumu kwa mujibu wa sheria ya uhamiaji ya Ujerumani.

Lindner amesema kubakia nchini Ujerumani lazima kuambatane na vigezo vinavyoeleweka badala ya kufuata mkumbo. Vigezo hivyo kwa waombaji ni pamoja na kuweza kujikimu kwa kufanya kazi, wawe hawajatenda uhalifu na waitambue katiba huru na ya kidemokrasia ya Ujerumani.