1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Euro2024: Mbappé kukosa mechi na Uholanzi

21 Juni 2024

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya kandanda ya Ufaransa, Kylian Mbappé, hatokuwepo katika kikosi cha mwanzo katika mechi ya leo usiku dhidi ya Uholanzi katika michuano ya Euro 2024 inayoendelea nchini Ujerumani.

https://p.dw.com/p/4hLxz
Euro 2024 l Austria vs Ufaransal Kylian Mbappe
Mchezaji wa timu ya taifa ya Ufaransa, Kylian Mbappe, baada ya kuumia pua kwenye michuano ya Euro 2024.Picha: Alessandra Tarantino/AP/picture alliance

Nyota huyo wa Ufaransa alivunjika pua katika mechi ya ufunguzi ya kundi D dhidi ya Austria ambapo Les Bleus walipata ushindi wa bao 1-0.

Mbappé hakuhitaji kufanyiwa upasuaji lakini atakuwa akivaa barakoa maalum.

Soma zaidi: Mbappe avunjika pua katika ushindi wa Ufaransa dhidi ya Austria

Kocha wa Ufaransa, Didier Deschamps, atalazimika kupanga upya safu ya ushambuliaji kwa kutegemea wachezaji kama Antoine Griezmann na Marcus Thuram.