1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Idadi ya vifo kufuatia mafuriko Ulaya ya Kati yaongezeka

19 Septemba 2024

Idadi ya waliofariki kutokana na mafuriko makubwa yaliyolikumba eneo la Kati na mashariki mwa Ulaya imeongezeka na kufikia angalau watu 23 huku makumi ya wengine wakiwa haijulikani walipo.

https://p.dw.com/p/4kpIi
Poland Lewin Brzeski mafuriko
Mafuriko Nchini Poland wakazi wanahamishwa na wafanyakazi wa dharura baada ya mto Nysa Klodzka kufurika mji wa Lewin Brzeski kusini-magharibi mwa Poland, Septemba 17, 2024.Picha: Beata Zawrzel/NurPhoto/IMAGO

Watu watano wameripotiwa kufariki katika Jamhuri ya Czech, ambapo rais wa nchi hiyo Petr Pavel ameyatembelea maeneo yaliyoathirika zaidi na mafuriko hasa mji wa mapumziko wa Jeseník. Hata hivyo hali ya wasiwasi kwenye mto Elbe karibu na mpaka na Ujerumani imepungua baada ya ujazo wa mto huo kutoongezeka baada ya kutokea dhoruba kali iliyosababisha mafuriko makubwa.