JangaMorocco
Idadi ya vifo yaongezeka Morocco na kukaribia watu 2,900
12 Septemba 2023Matangazo
Vikosi vya uokoaji vimeendelea bila kuchoka kuwatafuta manusura usiku kucha.
Morocco imekuwa ikikosolewa kuchelewesha kutoa idhini kwa mashirika mengine ya uokoaji kuingia nchini humo ili kutoa msaada.
Maafisa wa Morocco wanasema uamuzi huo unalenga kuepuka mkanganyiko katika uratibu ambao wanadai hautokuwa na manufaa yoyote.
Soma pia:Tetemeko la ardhi Morocco: Idadi ya vifo yakaribia 2,900
Ufaransa imetangaza msaada wa dharura kwa Morocco wa dola milioni 5.4 utakaolekezwa kwa mashirika ya kimataifa yasiyo ya kiserikali yanayoendelea kutoa msaada nchini humo.
Hili ni tukio baya zaidi kuwahi kuikumba nchi hiyoya Kaskazini mwa Afrika tangu tetemeko la ardhi la mwaka 1960 lililoharibu mji wa Agadir na kusababisha vifo vya maelfu ya watu.