Idadi ya watu waliopewa uraia wa Ujerumani yaongezeka
28 Mei 2024Matangazo
Idadi ya watu waliopewa uraia wa Ujerumani imeongezeka maradufu mwaka jana tangu rekodi za uraia zilipoanza kuchukuliwa mwaka 2000.
Ofisi inayohusika na takwimu imesema idadi hiyo imeongezeka kwa asilimia 19 ikilinganishwa na mwaka uliopita, kiwango hicho kikiwa tayari kimeongezeka kwa asilimia 28 mnamo mwaka 2022.
Ofisi hiyo imeeleza kuwa watu wapatao 200,100 walipata uraia wa Ujerumani mwaka jana 2023.
Watu kutoka mataifa 157 walipewa uraia wa Ujerumani mwaka jana, wengi wakitokea Syria, Uturuki, Iraq, Romania na Afghanistan.
Watu waliopewa uraia wa Ujerumani walikuwa na wastani wa umri wa miaka 29, ikimaanisha kuwa wengi walikuwa vijana.