IMF yaidhinisha mkopo wa dola milioni 786 kwa Tanzania
21 Juni 2024Matangazo
Bodi ya IMF imeipatia Tanzania fedha nyengine karibu dola milioni 150, baada ya kuafiki kuwa nchi hiyo imekamilisha vigezo muhimu chini ya mpango wa awali wenye thamani ya zaidi ya dola bilioni moja, ulioongezewa muda wa miezi sita zaidi hadi Mei mwaka 2026.
Soma zaidi:Zambia yaagizia maelfu ya tani za mahindi kutoka Tanzania
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa IMF, Bo Li, ameusifu utendaji wa Tanzania pamoja na ajenda yake ya mageuzi.
Kulingana na shirika hilo la fedha duniani, ukuaji wa uchumi wa Tanzania uliongezeka mwaka jana huku mfumuko wa bei ukidhibitiwa.