Kais athibitishwa kushinda asilimia 90.7 Tunisia
12 Oktoba 2024Matangazo
Matokeo hayo yaliyotangazwa jana, hayana tafauti kubwa na matokeo ya awali, ambayo yanampa fursa kiongozi huyo anayetawala kwa mkono wa chuma kutawala kwa muhula mwengine wa miaka mitano madarakani.
Vyama vya upinzani na makundi ya haki za binaadamu yamehoji uhalali wa matokeo hayo, ambayo yamepatikana baada ya wagombea waliokuwa madhubuti kuondoshwa kwenye uchaguzi wenyewe.
Soma zaidi: Rais wa Tunisia Kais Saied anatarajiwa kushinda muhula wa pili
Wagombea pekee walioruhusiwa kuwania walikuwa ni Ayachi Zammel, aliyetangazwa kupata asilimia 7.3 na Zouhair Maghzaoui aliyepata takribani asilimia 2.
Kwa ujumla, watu waliojitokeza kupiga kura walikuwa ni asilimia 28.8 tu ya wapiga kura wote halali.