1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kongo yatupilia mbali wito wa kurudia uchaguzi mkuu

29 Desemba 2023

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imetupilia mbali wito wa upinzani kutaka kurejewa uchaguzi wenye utata, baada ya ujumbe wa waangalizi wa Kanisa Katoliki kuripoti ''kasoro na udanganyifu'' katika uchaguzi

https://p.dw.com/p/4ahMj
Kinshasa, Kongo 2023 | Makao makuu ya CENI- | Didi Manara, Naibu Mwenyekiti CENI
Naibu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo CENI Didi Manara.Picha: Saleh Mwanamilongo/DW

Mkuu wa Kongamano la Maaskofu wa Kikatoliki nchini Kongo, Donatien Nshole, amesema ujumbe huo umegundua visa vingi vya ukiukwaji wa taratibu za upigaji kura ambavyo huenda vikaathiri usahihi wa baadhi ya matokeo.

Soma pia:Waangalizi uchaguzi wajizuia kutoa msimamo wa uchaguzi Kongo

Rais Felix Tshisekedi anayewania muhula wa pili ameonekana kupata kura zaidi ya milioni saba ambazo ni sawa na asilimia 77, huku mpinzani wake wa karibu Moise Katumbi akiwa na asilimia 15 na Martin Fayulu akishika nafasi ya tatu na asilimia 4 pekee.