Koopsman: Nitaendela kushinikiza suluhu ya mataifa mawili
20 Julai 2024Mjumbe wa amani wa Umoja wa Ulaya anayeshughulikia maswala ya Mashariki ya Kati Sven Koopsman amesema katika mahojiano na shirika la Habari la AFP, kwamba ataendelea kushinikiza hatua zitakazowezesha kupatikana suluhu ya mataifa mawili ya Israel na Palestina.
Soma zaidi. Ursula von der Leyen achaguliwa kuongoza tena Halmashauri ya Ulaya kwa miaka mitano
Koopmans amesema licha ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kupinga juhudi za kuundwa taifa huru la Palestina lakini yeye anaamini kuwa suluhu ya mataifa mawili bado inaweza kufikiwa.
Mjumbe huyo wa amani wa Umoja wa Ulaya anayeshughulikia maswala ya Mashariki ya Kati, amesema huku vita vya Gaza vikiendelea na Israel ikiwa inahitaji uungwaji mkono wa kimataifa, serikali ya Netanyahu haitakiwi kupuuza kwa muda usiojulikana maoni ya nchi za Ulaya juu ya kuutatua mzozo huo.
Soma zaidi.Zelensky asema atapinga mipango yoyote itakayofikiwa na Urusi bila ya kuwahusisha
Koopmans amesema kazi yake inaongozwa na tamko la Umoja wa Ulaya la mwaka 1980 linalotambua haki ya kuwepo taifa la Israel na usalama wake na pia haki kwa watu wa Palestina.