Korea Kusini yamwita balozi wa Urusi
21 Juni 2024Balozi Georgy Zinoviev anayeiwakilisha Moscow ameitwa na serikali ya Korea Kusini kwa ajili ya kutoa maelezo ikiwa ni sehemuj ya hatua ya Seoul kupingana na makubaliano kati ya Urusi na Pyongyang.
Serikali mjini Seoul imeitaka Urusi kuacha mara moja ushirikiano wa kijeshi na Korea Kaskazini na kuheshimu maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Soma zaidi: Putin kusaini mikataba ya ushirikiano wakati wa ziara mjini Pyongyang
Korea Kaskazini imekuwa chini ya vikwazo vya Umoja wa Mataifa tangu mwaka 2006 kutokana na mpango wake wa nyuklia uliopigwa marufuku.
Hatua hizo ziliungwa mkono na Urusi hapo awali, lakini Putin amesema vikwazo hivyo vinapaswa kupitiwa upya.
Putin ameionya pia Korea Kusini kuhusu azma yake ya kuipatia Ukraine silaha, na kusema hilo litakuwa kosa kubwa.