Mahama aongoza katika matokeo ya mwanzo ya kura, Ghana
8 Desemba 2024Matangazo
Shirika binafasi la televisheni la Joy limesema matokeo ya awali kutoka maeneo 25 kati ya 276 yanamuonesha Manama kiongozi wa chama cha National Democratic Congress (NDC) akiwa na asilimia 50.25 ya kura huku makamu rais Mahamudu Bawumia wa chama tawala cha New Patriotic Party NPP akiwa na asilimia 48.1 ya kura.
Wapiga kura milioni 18 wanamchagua rais nchini Ghana
Katika uchaguzi wa bunge NDC inaongoza ikiwa na viti 16 vya bunge huku chama tawala kikipata viti 9. Bunge la taifa hilo lina jumla ya viti 276.
Ghana ina historia ya utulivu wa kisiasa na vyama viwili vikuu vya NPP na NDC vimepishana madarakani kwa amani tangu nchi hiyo iliporejesha demokrasia ya vyama vingi manamo mwaka 1992.