Majeshi ya Israe yazingira miji ya Gaza
6 Januari 2009Majeshi ya Israel yaliendeleza mashambulizi yake dhidi ya Hamas katika miji ya ukanda wa Gaza yenye wakaazi wengi baada ya jeshi hilo kulizingira eneo hilo katika juhudi za kuwasaka wafuasi wa kundi la Hamas.
Mashambulizi hayo yaliyotekelezwa ardhini na angani yamejibiwa na mizinga ya roketi kutoka upande wa Hamas ambapo yaripotiwa wanmerusha zaidi ya Mizinga 10 ya Roketi katika ardhi ya Israel. Hali ilivyo katika eneo hilo inatajwa kuwa mbaya huku viongozi wa kimataifa wakiendelea na jjuhudi zao za kusitisha mapigano hayo.
Hali inayoshuhudiwa katika hospitali za ukanda wa Gaza kufuatia mashambulizi hayo ya usiku inatajwa kuwa mbaya ambapo yalimesababisha watu 22 kuuliwa huku mamia ya wengine kujeruhiwa na kuifikisha idadi ya watu waliouawa tangu mapigano hayo yaanze kuwa watu 573 na wengine 2,600 kujeruhiwa .
Miongoni mwa Watu wao waliouliwa 100 ni kina mama na watoto.
Shirika la kutoa misaada ya kibinadamu katika eneo hilo la Gaza linasema kuwa shambulizi la jeshi la Israel lililotekelezwa hivi punde katika shule moja ya inayoendeshwa na Umoja wa mataifa UNRWA iliyoko Magharibi mwa mji wa Gaza, inayowahifadhi wakimbizi 400 limewaua watu watatu waliokuwa wamekwenda kujisaidia.
Mashambulizi makali pia yameripotiwa katika eneo la kusini,Mashariki, na Kaskaini mwa mji huo wa Gaza ambao sasa umezingirwa na kusambaa hadi mji Khan Yunis na Jabiliya kaskazini mwa Gaza, ambako kuna kambi kubwa ya wakimbizi.
Mashirika ya misaada ya kibinadamu katika eneo hilo la Gaza yanasema kuwa iwapo mashambulizi hayo hayatakomeshwa,hali hiyo itazidi kuwa ngumu kwani tayari huduma za ambulensi zimeshindwa kuwafikia majeruhi wengi walioko katika maeneo hayo ya mapigano yaliyozingira.
Lakini rais wa Israel Shimon Peres amesema kuwa nchi yake itaendelea na mashambulizi hayo katika kutekeleza haki ya kuwalinda raia wake na haijali itakavyochukuliwa na jamii ya kimataifa.
Hali kadhalika Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Israel Israel Tzipi Livni amesema kuwa jeshi hilo la Israel halinabudi kuendeleza mashambulizi hayo mahali popote litakaposhuku kuwa maficho ya wafuasi wa Hamas ambao wameendelea kuishambulia Israel kwa mizinga ya roketi..
Athari za mapigano ya Gaza sasa zimeanza kutisha kusambaa hadi maeneo mengine baada ya wabunge nchini Afghanistan kutangaza kwamba zaidi ya vijana 2,000 nchini humo wako tayari kwenda Gaza kuwasaidia Wapalestina.
Hali kadhalika kuna habari kwamba mshambulizi wa kujitolea mhanga aliligongesha gari lake katrika lango la dhabahu moja mjini Toulouse nchini Ufanransa kisha kuliteketeza moto.
Rais Nicholas Sarkozy ambayo yuko eneo la mashariki ya kati ameshtumu kitendo hicho huku akitaka jamii ya kimataifa kushughulikia suala hilo kwa dharura.
Rais Sarkozy alisema haya baada ya kufanya mashauri na Rais wa Syria Bashar- Al Assad ambapo alimtaka rais huyo kufanya juhudi za kuwashinikiza Hamas kukomesha vita hivyo.
Kwa upande wake aliyekuwa waziri mkuu wa Uingezera Tonny Blair alisema kuwa njia pekee ya kukomesha mapigano hayo ni kufunga njia zote zinazotumiwa na Hamas kupata silaha zao.
Baraza la usalama la Umoja wa mataifa bado linaendelea na mazungumzo yake kuhusiana na mzozo huo,huku viongozi wanaohudhuria kikao hicho wakihimiza kuchunguzwa kwa makini mazingira yatakayopelekea kusitisha mapigano na kudumishwa kwa mkataba baina ya Israel na eneo la Gaza.