1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Makundi ya waasi Syria yakubali kuweka chini silaha

24 Desemba 2024

Utawala wa mpito wa Syria umesema makundi yote ya waasi yatavunjwa na kuunganishwa chini ya wizara ya ulinzi.

https://p.dw.com/p/4oYSt
Syrien Kämpfer der Syrian Democratic Forces SDF
Wapiganaji wa SDF baada ya waasi kuuteka mji mkuu na kumwondoa madarakani Bashar al-Assad wa Syria, huko Hasakah, Syria Desemba 11, 2024.Picha: Orhan Qereman/REUTERS

Viongozi wa makundi kadhaa ya waasi yamekubali hatua hiyo baada ya kuwa na mkutano na kiongozi mpya wa Syria, Ahmed al-Sharaa. Al-Sharaa ambaye zamani alijulikana kama Abu Mohammed al-Joulani - aliweka wazi kuwa hatokubali makundi yaliyojihami kufanya shughuli zao nje ya udhibiti wa serikali. Kundi lake la waasi la Hayat Tahrir al-Sham liliunda serikali ya mpito baada ya kuuangusha utawala wa Bashar al Assadmnamo Desemba 8. Syria imegawika tangu kuzuka kwa maandamano ya kuipinga serikali ya mwaka 2011 na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe.