1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani: Yaahidi msaada zaidi wa kijeshi kwa Ukraine

Zainab Aziz Mhariri: Babu Abdalla
25 Aprili 2022

Mawaziri wa ulinzi wa Marekani Lloyd Austin na wa Mambo ya Nje Antony Blinken walifanya ziara mjini Kyiv na kukutana na rais wa Ukraine Volodymir Zelensky na kuahidi msaada wa silaha ili kukabiliana na Urusi.

https://p.dw.com/p/4AO3O
Ukraine / USA - Treffen von Lloyd Austin, Antony Blinken und Volodymyr Zelenskyy
Picha: Ukrainian Presidential Press Service/REUTERS

Viongozi hao wamefanya ziara hiyo wakati vita vya nchini Ukraine vikiwa vimeingia katika mwezi wa pili kulekea wa tatu sasa, huku maelfu ya watu wakiuawa na mamilioni wengine wakilazimika kuyahama makaazi yao.

Mzozo huo umeyahusisha mataifa ya Magharibi kuungana katika kuiunga mkono Ukraine na hivyo dunia imekuwa inashuhudia silaha zikimiminika nchini humo.

Waziri wa ulinzi wa Marekani Lloyd Austin amesema kwa upande wao, wanaona hatua ya kwanza kwa Ukraine kuweza kushindavita hivi ni kuamini kuwa wana uwezo wa kushinda vita dhidi ya Urusi, halafu kitakachofuata baada ya kuamini ni kuhakikisha wanapata vifaa sahihi vya vita na pia msaada sahihi.

Waziri Austin amesema waukraine wanahitaji makombora ya masafa marefu na kwamba Marekani inafanya kila iwezalo kuwapa usaidizi wa aina hiyo wa mizinga na silaha ambazo zitakuwa na ufanisi mkubwa katika hatua hii ya mapambano.

Soma:Ukraine yapigwa tena; Zelenskiy asema maafisa wa Marekani kuzuru

Waziri Austin amesema Marekani inataka kuiona Urusi inadhoofika kwa kiwango ambacho haitoweza kufanya kile ilichokifanya nchini Ukraine na pia kuizuia kuanzisha mashambulizi zaidi katika siku zijazo.

 

Blinken: Azungumza na Guterres kuhusu mzozo wa Ukraine

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken amesema amezungumza na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ambaye atakwenda mjini Moscow mapema wiki hii.

Amesema ana matarajio kwamba atawasilishaujumbe mkali na wa wazi kwa rais wa Urusi Vladimir Putin, kuhusu haja ya kuvimaliza vita hivi haraka.

Blinken amesema rais Zelensky amejitolea kushinda vita vya nchi yake dhidi ya Urusi na kwamba Marekani itamsaidia kulifikia lengo hilo.

 

Marekani yafadhili Ukraine silaha za kivita za kisasa

Marekani ndiye mfadhili mkuu wa fedha na silaha wa Ukraine na inaongoza kwa kuweka vikwazo dhidi ya Urusi, lakini ilikuwa bado haijawapeleka maafisa wowote wa juu nchini humo tangu vitavianze, wakati viongozi kadhaa wa Ulaya wamekuwa wakienda huko kusisitiza uungaji mkono wao.

USA Ukraine Diplomatie l Außenminister Antony Blinken in Washington
Waziri wa mambo ya nje Marekani Antony BlinkePicha: Susan Walsh/Pool/AFP

Mawaziri wa Marekani Austin na Blinken wamesema wanadiplomasia wa Marekani wataanza kurejea nchini Ukraine kuanzia wiki hii na wametangaza msaada wa dola milioni 700 kama msaada wa ziada wa kijeshi kwa Ukraine.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken alipanda ndege kurejea Marekani kutoka Poland Jumatatu baada ya yeye na Waziri wa Ulinzi Lloyd Austin kukamilishaziara ya siri ya mjini Kyiv, ambapo walikutana na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky.

Shinikizo laongezeka kwa Ujerumani kutuma silaha nzito Ukraine