1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroSudan

Mashambulizi ya siku mbili ya RSF El-Fasher yaua watu 48

28 Septemba 2024

Siku mbili za mashambulizi ya wanamgambo wa Sudan wa RSF katika mji wa El-Fasher yamesababisha vifo vya watu 48.

https://p.dw.com/p/4lBar
Uharibifu kutokana na mashambulizi huko El-Fasher
Uharibifu kutokana na mashambulizi huko El-FasherPicha: AFP

Kwa muhibu wa mamlaka za kiafya huko El-Fasher, mashambulizi ya jana pekee yalisababisha vifo vya watu 30 na kuwajeruhi makumi ya wengine. Jeshi la Sudan na wanamgambo wa RSF wanawania kuudhibiti mji huo mkuu wa jimbo la Darfur Kaskazini.

Hayo yanajiri wakati viongozi wa dunia wakitoa wito wa kukomesha vita nchini humo. Vita kati ya mkuu wa jeshi Abdel Fattah al-Burhan na kiongozi wa RSF Mohamed Hamdan Daglo vimeua makumi ya maelfu ya watu.

Soma pia: Pande hasimu nchini Sudan zakubali mazungumzo ya kusaka amani

Shirika la Afya Duniani WHO limetaja idadi ya vifo kuwa ni watu wasiopungua 20,000 lakini mjumbe wa Marekani nchini humo Tom Perriello amesema makadirio mengine yanaeleza kuwa vifo vimefikia 150,000.