1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiAfrika

Misri kurejea kuchimba gesi asilia

20 Septemba 2024

Serikali ya Misri imetangaza kuwa inatarajia mwakani mnamo majira ya joto, kuanzisha tena mchakato wa uchimbaji wa gesi asilia ambayo inategemewa kwa kiasi kikubwa ili kuzalisha umeme.

https://p.dw.com/p/4kt9n
Baraza la mawaziri la Misri.
Baraza la mawaziri la Misri.Picha: EGYPTIAN PRESIDENCY/AFP

Waziri Mkuu Mostafa Madbouly aliwaambia waandishi habari kwamba uchimbaji umeshuka kwa sababu ya malimbikizo ya madeni ambayo serikali inatarajia kuyalipa makampuni ya uchimbaji.

Hata hivyo, Madbouly hakutaja ni kiasi gani serikali inadaiwa wala wakati inaotarajia kulipa madeni hayo.

Soma zaidi: Misri yaandaa mkutano kuyakutanisha makundi ya kisiasa ya kiraia ya Sudan kwenye

Mwezi Machi, shirika la habari la Reuters lilielezwa na vyanzo vyake kuwa serikali ilitenga hadi dola bilioni 1.5 ili kuyalipa makampuni ya kigeni ya kuzalisha mafuta na gesi yanayofanya kazi nchini humo.

Malimbikizo ya madeni yaliongezeka wakati Misri ilipokabiliwa kwa muda mrefu na uhaba wa fedha za kigeni ambao kwa sasa umepungua.