1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiAfrika

Mkutabo wa mwaka wa IMF na Benki ya Dunia wafanyika Afrika

9 Oktoba 2023

Wajumbe wa Shirika la Fedha la Kimataifa, IMF, na Benki ya Dunia kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 50 wanafanya mkutano wao wa kila mwaka katika ardhi ya Afrika huko nchini nchini Morocco.

https://p.dw.com/p/4XHyO
USA IWF Pierre-Olivier Gourinchas
Wajumbe wa IMF wakiwa katika mkutano wa kawaida kujadili uchumi wa duniaPicha: Liu Jie/Xinhua/IMAGO

Mkutano huo unaofanyika leo Jumatatu unakabiliwa na shinikizo la kufanya mageuzi kwa ajili ya kuyasaidia mataifa maskini yaliyoathiriwa na madeni na mabadiliko ya hali ya hewa.

Kwa kawaida, IMF na Benki ya Dunia huwakutanisha mawaziri wa fedha kwenye mkutano wa kila mwaka na magavana wa benki kuu kila baada ya miaka mitatu nje ya makao makuu yaliyoko mjini Washington, Marekani.

Soma pia:IMF yaipa Burkina Faso mkopo wa dola milioni 302

Jiji la kusini mwa Morocco la Marrakesh lilipaswa kuwa mwenyeji wa mkutano huo mnamo mwaka 2021, lakini uliahirishwa mara mbili kwa s+ababu ya janga la UVIKO-19.

IMF na Benki ya Duniazilifanya mikutano barani Afrika mara ya mwisho mnamo mwaka wa 1973, ambapo Kenya iliandaa hafla hiyo.