Mzozo kati ya Urusi na Ukraine ambao unaelekea kuingia katika mwaka wa tatu unazidi kutokota. Mwishoni mwa mwezi Agosti, mawaziri wa ulinzi wa Umoja wa Ulaya walijadiliana kuhusu kuongeza msaada wa kijeshi kwa Ukraine. Lakini pia mzozo huo umezusha hali ya hofu kwa mataifa ya Baltic yanayopakana na Urusi ambayo yanahofia kwamba wakati wowote wanaweza pia kushambuliwa. Ungana na Bakari Ubena.