Nigeria yaizika Ghana na kutinga michuano ya CHAN 2025
30 Desemba 2024Matangazo
Nigeria na Ghana zimewahi kukutana mara mbili katika mechi za kufuzu CHANna katika kila mchezo, Waghana waliibuka washindi. Aidha Cote d'Ivoire na Mali hazikupata tiketi ya kucheza michuano hiyo itatakayoandaliwa nchini Kenya, Tanzania na Uganda Februari mwakani. Itakuwa mara ya kwanza kwa Jamhuri ya Afrika ya Kati, inayoorodheshwa nafasi ya 135 duniani, kushiriki katika michuano hiyo ya CAF. Cote d'Ivoire iliangushwa na Burkina Faso mjini Bamako. Mali, washiriki katika mashindano matano kati ya saba yaliyopita ya CHAN, ilibanwa na Mauritania iliyojikatia tiketi.