Poland kuzungumza na Ukraine juu ya usafishaji nafaka
27 Septemba 2023Matangazo
Hayo yameelezwa hii leo na waziri wa kilimo wa Poland Robert Telus muda mfupi baada ya kufanya mkutano na mwenzake wa Ukraine Mykola Solsky.
Telus ameyasifu mazungumzo hayo akiyataja kuwa njia muhimu ya kutatua tofauti zilizojitokeza kati ya nchi yake na Ukraine.
Soma pia:Makombora ya Urusi yamjeruhi mtu mmoja katika bandari ya Odessa nchini Ukraine
Mahusiano kati ya Ukraine na Poland yameingia doa baada ya Poland pamoja na nchi nyingine mbili za Umoja wa Ulaya za Hungray na Slovakia kuamua kurefusha marufuku ya usafirishaji nafaka za Ukraine kupitia ardhi zao.
Uamuzi huo ulifikiwa kufuatia madai kwamba mazao ya Ukraine yaliyo njiani kwenda soko la kimataifa huuzwa kinyemela ndani ya mataifa hayo matatu na kuwaumiza wakulima wa ndani.